Wazazi waliokatisha watoto masomo kukamatwa
17 March 2023, 4:04 pm
Baadhi ya wazazi wanadai elimu zote mbili zina umuhimu huku wengine wakibainisha kuwa walimu pia wanachangia kuongeza kwa utoro shuleni.
Na Nizar Khalfan.
Zoezi la ukamataji la wazazi wa wanafunzi watoro limeanza wilayani kondoa ambapo zaidi ya wazazi kumi na mbili wamekamatwa huku wakidaiwa kuwaachisha wanafunzi hao masomo na kuwapeleka madrasa kujifunza elimu ya Dini
Wakizungumza na dodoma fm Baadhi ya wakazi wa wilaya ya KONDOA wamesema elimu zote mbili zina umuhimu huku wengine wakibainisha kuwa walimu pia wanachangia kuongeza kwa idadi ya utoro shuleni
Nae mtendaji wa kata ya KONDOA mjini Samson Godfrey Mtui amesema zoezi Hilo limeanza na tayari zoezi la kuwapeleka wazazi hao mahakamani huku watoto hao wametakiwa kuanza kuhudhuria Masomo kuanzia march 28 mwka huu.