TASAC yakanusha madai ya rushwa kwa CMA
13 March 2023, 8:52 am
Suala hilo ni miongoni malalamiko matatu yaliyoripotiwa kupitia mitandao ya kijamii ambapo pia kupitia mitandao hiyo vijana hao wamelalamikia kuvunjwa kwa mikataba bila ya kufuata utaratibu na kufanya kazi bila ya bima ya afya.
Na Mindi Joseph.
SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC),limewahakikishia watanzania kuwa haijawahi kutoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA),ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na vijana waliokuwa wanafanya shughuli za mafunzo kazi kwa vitendo ndani ya shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Abdi Mkeyenge amesema shirika hilo lilikuwa likitekeleza majukumu yake kupitia vijana waliokuwa wameajiriwa moja kwa moja na waliokuwa wanafanya mafunzo ya kazi lakini kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na bunge mnamo Julai mwaka jana ilililazimu shirika hilo kuvunja mikataba kwa vijana 209 na sio zaidi ya 400 kama ilivyoripotiwa.
Akitoa ufafanuzi kuhusu vijana hao 209 waliofutiwa mikataba Mkeyenge amesema kati yao vijana 41 ndio hawakuridhika na maamuzi hayo hivyo kutoa wito kwa umma kuwa na subira wakati Tume inapofanyia kazi mashauri hayo.
Julai mwaka jana,Bunge lilifanya mabadiliko ya Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania kwak ufuta majukumu ya kipekee ya uwakala wa meli,uhakiki wa mizigo,udhibiti wa nyaraka na kupunguza wigo wa jukumu la kufnaya uwakala wa forodha katika bidhaa zilizokuwa zinagombewa na kuondoshwa TASAC ambapo kupitia mabadiliko hayo Shirika hilo lilivunja mikataba kwa vijana hao