Wananchi walia na uhaba wa Miundombinu ya Umeme Chiboli
24 February 2023, 4:19 pm
Jografia ya kijiji hicho cha Champumba imekuwa na changamoto katika kusambaza nguzo za umeme licha ya kupewa ahadi ya kusubiri awamu inayofuata.
Na Victor Chigwada.
Kukosekana kwa Miundombinu ya Umeme ikiwemo Nguzo za Kutosha katika Kata ya Chiboli Wilaya ya Chamwino ni sababu inayosababisha wananchi katika baadhi ya Vitongoji kushindwa kunufaika na nishati hiyo
Hali hiyo imetusukuma kuzungumza na Diwani wa Kata Chiboli Bw.Wiliamu Teu ambaye amesema changamoto hiyo ni kilio cha muda mrefu ambapo Mwaka jana walifanikiwa kuunganishia huduma ya umeme
Amesema kuwa licha ya huduma hiyo kuwafikia lakini changamoto iliyoibuka ni kuhusu usambazaji wa nguzo za umeme kusuasua na baadhi ya maeneo kwa kutofikiwa na huduma hiyo
Aidha ameiomba Serikali kupitia mamlaka husika kushughulikia changamoto hiyo ili wananchi waweze kunufaika na nishati hiyo ikiwemo kujiletea maendeleo
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji amesema kuwa katika kijiji hicho kuna vitongoji vitano huku vitongoji viwili vikiwa vimefanikiwa kuunganishiwa huduma ya Umeme