Mkandarasi ahimizwa kuharakisha ujenzi wa bwawa Membe
6 February 2023, 2:06 pm
Mradi huo wa Bwawa la umwagiliaji unagharimu shilingi Bilioni 12 na litakapokamilika litachukua eneo lenye ukubwa wa ekari 388 na linatarajiwa kumwagilia mashamba yenye eneo la ukubwa wa ekari 8,000.
Na Fred Cheti.
Ujenzi wa Mradi wa bwawa kubwa la Kumwagilia katika Kata ya Membe wilayani Chamwino unatarajia kuongeza tija ya kilimo kwa wakulima wilayani humo ambao wanatagemea mvua pekee katika kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule hivi karibuni alifanya ziara yake wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo alipongeza juhudi zinazoendelea katika ujenzi wa bwawa hilo huku akimtaka makandarasi kuongeza kasi katika ujenzi wa bwawa hilo .
Nae Msimamizi wa ujenzi wa Bwawa hilo kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji anaelezea mradi huo hatua ulipofikia mpaka sasa na lini unatarajia kukamilika.
Kwataarifa zaidi bonyeza hapa.