Ukubwa wa riba kikwazo kwa wakopaji mikopo
16 November 2022, 12:19 pm
Na; Eva Enock.
Imeelezwa kuwa ukubwa wa riba pamoja na elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo ni miongoni mwa sababu zinazopelekea baadhi ya watu kushindwa kurejesha mikopo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi jijini Dodoma wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusiana na nini sababu inayopelekea baadhi yao kushindwa kunufaika na fedha za mikopo ambapo wamesema jamii haina elimu ya kutosha juu ya mikopo hivyo kusababisha wengi wao kushindwa kunufaika na mikopo wanayo chukua.
.
Wameiomba serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisjha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya mikopo kabla ya kuchukua mikopo hiyo
kwa upande wake meneja wa benki ya TCB kanda ya kati Bw. Edward Mlowo anasema kuwa benki ama taasisi za kifedha zinao wajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa wateja wao kabla ya kumpatia mkopo huku akiwasihi wananchi kuachana na tabia ya kuchukua mikopo bila ya kujipanga na kuwa na kusudio maalum.
.
Mikopo imekuwa na umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara kwani imekuwa ikiwawezesha katika kupata fursa ya kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi.