Miganga walalamikia ubovu wa Barabara
12 October 2022, 11:04 am
Na; Benard Filbert.
Wakazi wa kijiji cha Miganga wilayani Chamwino wamelalamikia Ubovu wa miundombinu ya Barabara kuwa kero inayosababisha baadhi ya huduma za msingi kupatikana kwa tabu.
Hayo yameelezwa na wakazi wa kijiji hicho wakati wakizungumza na Taswira ya habari mahojiano maalumu kuhusu hali ya miundombinu katika mchango wa maendelea katika kijiji cha Miganga
Baadhi yao wamesema ni vyema serikali ingeangalia namna bora ya kuboresha barabara hiyo ili kupunguza adha ambazo zinawakumba hususani kipindi cha masika.
CLIP WANANCHI……………….01
Taswira ya habari imezungumza na mwenyekiti wa kijiji cha Miganga Bw John Mawaya ambapo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akieleza hatua zinazochukuliwa ili kutatua changamoto ya ubovu wa barabara hiyo.
CLIP MWENYEKIT………………..02
Barabara ya Miganga kwenda Mvumi Mission katika wilaya ya Chamwino ni barabara ambayo imekuwa ikitumika na wakazi hao licha yakutokuwa rafiki kwao.