Wenyeviti Njoge walia na posho
5 October 2022, 2:06 pm
Na ;Victor Chigwada.
Licha ya kufunguliwa akaunti za Benki kwa ajili ya kulipwa Posho ,bado hakuna hatua iliyochukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa malipo hayo kwa Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji.
Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji ni miongoni mwa viongozi wanaofanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na malalamiko ya changamoto mbalimbali
Suala la Posho kwa ajili ya kuwapunguzia baadhi ya changamoto bado limekuwa kizungumkuti na halina suluhu.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Makutupa Kata ya njoge Bw.Peter Mwachahe amesema kuwa kwa hivi karibuni walipata matumaini kidogo baada ya kuambiwa wafungue akaunti za malipo ya posho lakini mpaka Sasa hakuna kinacho endelea
.
Naye Diwani wa kata hiyo Bw.Abdalla Dedu amekiri kupokea taarifa za wenyeviti kufunguliwa akaunti za malipo ndani ya kata yake lakini hakuna mafanikio yoyote katika utekelezaji
Dedu amesema kuwa suala la posho ya kujikimu kwa viongozi hao lingesaidia kupunguza hata masuala ya rushwa kwa baadhi ya viongozi kutokana na viongozi hao kuwa karibu na wananchi
.
Deo Ndejembi ni mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti Dodoma mjini ameiomba Serikali kuhakikisha wanawaboreshea posho zao na kuwafungulia akaunt za benki ili kupunguza kupanga foleni kwenye madirishani ya Malipo.
.
Hata hivyo Mwishon mwa mwaka 2021 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde wakati alipokuwa anazindua Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Serikali kuwekewa utaratibu kwa kila Mtaa au Kijiji kulipa posho kutokana na mapato yao.