Hifadhi ya swagaswaga kuendelea kuboresha miundombinu kwaajili ya watalii
10 August 2022, 2:18 pm
Na; Benard Filbert.
Uongozi wa hifadhi ya pori la akiba Swagaswaga wilayani Chemba mkoani Dodoma amesema unaendelea kuboresha miundombinu ya hifadhi hiyo lengo kuandaa mazingira rafiki kwa watalii.
Hayo yameelezwa na Donard Shija Mkuu wa Kitengo cha Ujirani mwema kutoka hifadhi ya pori la Swagaswaga wakati akifanya mahojiano na Dodoma fm kuhusu hifadhi hiyo.
Amesema muitikio wa watalii kuja katika hifadhi hiyo ni mzuri ikilinganishwa na kipindi cha nyuma
Kadhalika amesema hivi sasa wanajenga kituo cha kupokea wageni kitakachokuwa kinabeba taarifa ambazo zinahusu hifadhi hiyo.
.
Hata hivyo amesema kwa mtu yeyote ambaye ataenda katika mbuga ya Swagaswaga atakutana na utamaduni wa watu wa kabila la wasandawe ,wanyama mbalimbali pamoja na uoto wa asili uliopo katika hifadhi hiyo
.
Hifadhi ya pori la akiba Swagaswaga inapatikana katika wilaya ya Chemba umbali wa kilomita 143 kutoka uelekeo wa Dodoma mjini.