Makulu waishukuru serikali kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa barabara
20 June 2022, 2:03 pm
Na; Alfred Bulahya.
Uongozi wa kata ya Dodoma makulu jijini Dodoma umeishukuru Serikali kwa kuwapatia bilioni 10 na milioni 300, kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, inayounganisha eneo la Chaduru, Njendegwa mashariki, Njedengwa magharibi, Medeli, Mwangaza na Bwawani.
Akizungumza leo na Taswira ya habari kwa niaba ya uongozi huo diwani wa kata hiyo bw, Fadhili Hosea Chibago amesema kuwa mradi huo utakwenda kuponesha kidonda cha muda mrefu kwa wananchi wa kata hiyo na kwamba itasaidia kuchagiza maendeleo.
Katika mradi huo amebainisha siri ya mafanikio ya kupata fedha hizo kuwa ni ushirikishwaji mzuri kutoka kwa wananchi huku akiwahakikishia wananchi waliopitiwa na mradi huo kulipwa stahiki zao kwa wakati.
Huu ni muendelezo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini ili kuondoa adha hiyo kwa wananchi wake.