Dodoma FM

Ongezeko la bajeti laleta tumaini katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji

22 April 2022, 1:32 pm

Na;Mindi Joseph.

Serikali imesema ina matarajio makubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Kilimo cha  Umwagiliaji  kutokana na ongezeko kubwa la Bajeti ya fedha za miradi ya Maendeleo kwa  Mwaka wa fedha 2022 – 2023.

Hayo yamesemwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  Bw. Reymond Mndolwa  wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Leo jijini Dodoma ambapo amesema hatua hii ya Serikali ina lenga kuongeza uzalishaji wa Mazao ya chakula na Biashara.

Ameongeza kuwa Serikali imeongeza kiasi cha fedha Shillingi Bilioni 146.5 Katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kuwataka watumishi wa Tume hiyo kuzingatia weledi katika maeneo yao ya kazi.

.

Bw. Mndolwa ameongeza kuwa watumishi wanao wajibu wa kuhakikisha wanatunza mali zote za Tume akitolea mfano magari na Mitambo inayotumika katika shughuli za ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji.

.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mara ya kwanza amefanya Kikao na watumishi wa tume hiyo  baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan mapema Mwezi huu.