Wakazi wa Dodoma watakiwa kutoa ushirikiano ili kumaliza changamoto ya maji
11 April 2022, 3:32 pm
Na; Shani Nicolous.
Wanachi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wadau wote wa maji wametakiwa kuendeleza ushirikiano na mamalaka ya maji safi na usafi wa mazingira Duwasa ili kufikia lengo la kumaliza changamoto ya maji.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka na usafi wa mazingira Singida SUWASA Bw. Sebastiani Warioba ambaye alikuwa ni Afisa uhusiano kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA .
.
Amesema serikali ipo mbioni kuhakikisha inatafuta fedha kwaajili ya kumaliza changamoto ambapo kwa upande wa maji taka tayari taratibu zote zimefanyika kuhakikisha miradi mikubwa inafanyika katika maeneo tofauti mkoani hapa.
.
Ameongeza kuhusu maji safi miradi mingi imefanyaika na inaendelea kufanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maji hivyo wananchi watarajie kupata maji yakutosha Dodoma .
.
Bw. Warioba ambaye ambaye alikuwa Afisa Uhusiano kutowa Duwasa ametoa shukurani kwa wananchi jijini hapa kwa ushirikiano na kuwasihi wananchi wa Singida watarajie utumishi uliotukuka kutoka kwake maadam watampa ushirikiano.