Dodoma FM

Wajawazito watakiwa kuzingatia lishe

11 April 2022, 2:44 pm

Lishe Hafifu kwa Mama wajawazito imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa Watoto kuzaliwa wakiwa na upofu wengine uoni Hafifu.

Taswira ya habari imezungumza na Daktari wa macho Wilaya Bahi Dk Fortunatus Nkane ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Macho Wilayani humo amesema Mama wajawazito walio wengi hawazingatii lishe Bora wanapokuwa wajawazito pasipo kutambua madhara yatakayompata mtoto.

 

.

Kufuatia Changamoto Hiyo Dkt Nkane amewahimiza mama Wajawazito kuzingatia lishe bora na kufika kliniki kwa wakati.

.

Tatizo la watoto kuzaliwa na upofu na uoni hafifu lipo kwa ukubwa gani, Taswira ya habari imezungumza na Richard Jinasa Mratibu wa Mradi wa afya ya kanda ya kati Dodoma amesema watoto zaidi ya elfu ishirini na Nne wamepatiwa matibabu  ya macho katika shule 47 za Mkoa wa Dodoma.

.

Jitihada za kukabiliana na upofu katika Mkoa wa Dodoma kupitia wadau mbalimbali zinaendelea.