Maduka ya Dawa yaliyopo mita 500 kutoka hospitali yatakiwa kuondoewa
26 January 2022, 3:58 pm
Na; Benard Filbert.
Baadhi ya wadau wa afya wanaomiliki maduka ya dawa karibu na Hospitali za Serikali wametakiwa kuachana na vitendo vya hujuma kutokana na kutopatikana baadhi ya dawa ndani ya Hosptali huku zikipatikana kwenye maduka yao.
Wito huo umetolewa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt.Alon Urio wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu maamuzi ya waziri wa afya ya kuondolewa kwa maduka ya afya yaliyopo mita 500 kuzunguka Hospitali za Serikali.
Dkt.Urio amesema hakuna mtu yeyote ambaye anazuiwa kuwa na duka tatizo linatokea pale baadhi ya wataalamu wa afya wanapoihujumu Serikali ili kukuza maduka yao.
Hivi karibuni Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu alitoa agizo la kuondolewa kwa maduka yote ya dawa ambayo yapo mita 500 ndani ya eneo la hospitali za Serikali kwa kile kinachodaiwa kuhujumu upatikanaji wa dawa katika hospitali hizo.