Wakulima wa kanda ya kati washauriwa kuandaa mbegu zinazo stahimili ukame
2 November 2021, 11:28 am
Na; Benard Filbert.
Kufuatia taarifa za mamlaka ya hali ya hewa msimu huu kuwa na mvua chini ya wastani kanda ya kati wakulima wameshauriwa kuandaa mbegu zinazoendana na hali hiyo.
Hayo yameelezwa na mkuu wa idara ya kilimo wilaya ya Kondoa bwana Hassani Kiseto wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu taarifa za uwepo wa mvua chini ya wastani.
Amesema ni vyema wananchi wakaangalia mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Ameongeza kuwa kinachofuata hivi sasa ni mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi jinsi ya kukabiliana na kiwango hiki cha mvua pasipokuwa na athari.
Wataalamu wa kilimo wanatakiwa kuongea na wakulima juu ya mbinu bora ya kufanya kilimo kinachoendana na mvua ya chini ya wastani.