EWURA yatangaza kupunguza tozo nane kwaajili ya kuwaletea unafuu wananchi
6 October 2021, 12:57 pm
Na; Mindi Joseph .
Mamlaka ya Nishati na Maji EWURA imetangaza kupunguza Tozo nane kwa ajili ya udhibiti wa EWURA na kuwaletea Unafuu wananchi.
Akizungumza na Taswira ya habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema wamefanya marekebisho hayo ya tozo mbalimbali Kufuatia Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhandisi Chibulunje amesema Serikali imebadilisha tozo ya matumizi ya miundombinu ya bandari ambayo inatozwa kwa Dola za Marekani (kwa tani na sasa itatozwa kwa shilingi ya Tanzania.
Aidha Serikali imepunguza tozo ya TRA ya kuchakata nyaraka kutoka shilingi 4.8 kwa lita na kuwa kiwango maalum cha shilingi milioni 20 kwa kila meli ambapo kwa wastani meli saba huleta shehena ya mafuta kila mwezi.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wakiwemo wamiliki wa vyombo vya usafiri ndani ya Jiji la Dodoma wamesema hatua ya kupunguzwa kwa tozo katika bidhaa za mafuta ni mwanzo mzuri wa wao kujiinua kiuchumi kutokana na kazi za usafirishaji wa abiria.
Serikali imepunguza gharama za kuweka vinasaba kwenye mafuta kutoka shilingi 14 kwa lita hadi shilingi 7 kwa lita.