Ukosefu wa Maabara wapelekea wanafunzi kushindwa kufaulu masomo yao
5 October 2021, 11:04 am
Na;Mindi Joseph .
Ukosefu wa maabara kwa baadhi ya shule za sekondari imetajwa kuwa changamoto kwa wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule zinazokabiliwa na changamoto ya miundombinu ya shule ambapo wamesema hali hiyo inawanyima fursa za kujifunza zaidi kwani baadhi ya shule mpaka sasa hazina maabara.
Afisa Elimu sekondari jiji la Dodoma Mwl Pendo Rweyemamu amesema katika bajeti ya Mwaka 2021 na 2022 milion 490 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa maabara huku milion 220 zimetengwa kwa ajili ya viti meza ili kuendelea kuboresha miundobinu ya shule.
Mkoa wa Dodoma unaendelea na jitihada za kuboresha elimu ili kuendelea kuongeza ufaulu kwa shule za sekondari hususani za serikali.