Watu 549 Mkoani Dodoma wapatiwa elimu ya Saikolojia
30 September 2021, 1:11 pm
Na;Mindi Joseph.
Watu 549 Mkoani Dodoma wamepatiwa elimu ya saikolojia kutokana na kukabiliwa na Tatizo la saikolojia ya Maisha ambayo inaendelea kuwakabili watu mbalimbali nchini.
Kwa kipindi cha miezi 6 kuanzia junuary hadi june mwaka huu 2021 watu 549 wamepatiwa huduma na asasi ya saiko senta kutokana na kukabiliwa na tatizo la saikolojia ya maisha.
Taswira ya habari imezungumza na Katibu Mtendaji Mkuu wa asasi ya Saiko Senta Sylivia Siriwa anatueleza maana ya saikolojia.
Ameongeza kuwa Tatizo la saikolojia huchangiwa na Mfumo wa maisha ya kila siku ya binadamu.
Katika maisha tunayoishi saikolojia ya maisha inaendelea kuwa changamoto kwani watu wengi hujikuta wakifanya ua kuishi maisha ambayo hayana uhusiano halisi na jinsi mtu anavyotakiwa kuishi hali hii hupelekea mtu kukubwa na tatizo la saikolojia.