Juhudi zahitajika ujenzi wa barabara katika kata Ibihwa
24 September 2021, 9:50 am
Na; Benard Filbert.
Licha ya wakala wa barabara za Mijini na Vijini TARURA Wilaya ya Bahi kuanza ujenzi wa barabara katika kata ya Ibihwa Wilaya ya Bahi imeelezwa bado juhudi zinatakiwa ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa kero kwa wananchi hususuani kipindi cha mvua.
Hayo yanajiri kufuatia ubovu wa miundombinu ya barabara katika kata hiyo hali ambayo imekuwa ikipelekea usumbufu kipindi cha mvua.
Mwijuki Benjamin ni diwani wa Kata ya Ibihwa ameiambia taswira ya habari kuwa tayari TARURA wameanza ukarabati wa barabara tangu mwezi wa 6 kuanzia Ibihwa kwenda Mkola na nusu yake wamekamilisha huku wakitarajia kuanza tena awamu nyingine mwezi huu mwishoni.
Amesema sehemu ambayo TARURA wameanza na ukarabati ni kutokana na vipaumbele vya huduma muhimu za kijamii kama afya na elimu ili wananchi waweze kufika sehemu hizo kwa urahisi.
Endapo barabara zilizopo katika Kata ya Ibihwa zikikamilika zitasaidia kuondoa usumbufu ambao wananchi wamekuwa wakikutana nao hususani msimu wa mvua ambapo inakuwa changamoto kubwa kupitika.