Wadau waiomba serikali kuwahusisha vijana na makundi maalum dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
23 September 2021, 11:22 am
Na; Nadhiri Hamisi.
Wadau wa utunzaji wa mazingira Nchini wameiomba Serikali kuwahusisha vijana na makundi maalum katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira.
Wakizungunza na Dodoma fm Neema Mwaikyusa mtaalamu wa mazingira na Bw. Sudi Salum mwanafunzi na mwanaharakati wa mazingira katika chuo kikuu cha mzumbe Mkoani Morogoro wamesema kuwa vijana ndiyo kundi linalotakiwa kupewa kipaumbele katika harakati za utunzaji wa mazingira ili kuongeza ufanisi zaidi
Aidha wadau hao wameongeza kuwa Serikali inapaswa kuondoa mianya yote iliyopo katika suala la utunzaji wa mazingira kwa kuongeza utoaji wa elimu kwa jamii zote za mijini na vijijini pamoja na kuboresha sheria zitakazodhibiti uchafuzi wa mazingira.
Mapema wiki hii katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutteres alizitaka Nchi zenye kipato kikubwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za tokomeza uchafuzi wa mazingira na kuzitaka Nchi wanachama kuwahuisisha zaidi vijana katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.