Wizara ya Afya imesema inaendelea kuboresha suala la upatikanaji wa vyeti njia ya TEHAMA kwa waliopatiwa chanjo
3 September 2021, 1:03 pm
Na;Yussuph Hans.
Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto imesema inaendelea kuboresha suala la upatikanaji wa vyeti Kwa njia ya TEHAMA kwa waliopatiwa chanjo ya UVIKO-19 ambapo Hadi Sasa imewapatia Mafunzo watoa huduma zaidi ya 1994.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi wakati akitoa ufafanuzi wa upatikanaji wa vyeti vya kielektroniki Kwa watu waliochanja.
Sanjari na hayo Dkt Subi Amewahimiza wananchi kupata chanjo ikiwa ni Kinga ya Uviko 19 kwani ni salama pamoja na kuzingatia afua zote za Kinga ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kuvaaa barakoa na kutumia vitakasa mikono.
Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wakazi Mkoani hapa na wamepongeza hatua hiyo ambapo wamesema suala hilo litaharakisha zaidi upatikanaji wa vyeti hivyo.