Wananchi waaswa kuacha tabia ya kutelekeza wagonjwa hospitali
30 August 2021, 1:38 pm
Na; Mariam Kasawa.
Watu wanaotelekeza wagonjwa hospitali kwa sababu ya kutokumudu gharama za matibabu wameshauriwa kutokufanya hivyo na badala yake wafike katika ofisi za ustawi wa jamii katika hospitali aliyolazwa mgonjwa ili kupata msaada.
Afisa ustawi wa jamii hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Paschazia Mboje amesema wamekuwa wakipewa taarifa za wagonjwa waliotelekezwa hospitali na kulibeba jukumu hilo mpaka mgonjwa atakapopona .
Amesema kumtelekeza mgonjwa ni moja ya ukatili kwa wagonjwa na umekuwa ukileta na madhara kwa mgonjwa hata kusababisha kutokupata afueni mapema kutokana na msongo wa mawazo.
Nae mtaalamu wa saikolojia Dorini amesema ni vizuri kwa familia akitokea mgonjwa wa muda mrefu kumtafutia group za watu wenye magonjwa kama yake ili kumsaidia kupunguza mawazo na kujiona bado ananafasi katika jamii yake .