Dodoma FM
Mradi wa kufua umeme Zuzu watajwa kufikia asilimia 98.
26 August 2021, 1:44 pm
Na;Mindi Joseph .
Mradi wa kituo cha kufua umeme Zuzu umetajwa kufikia asilimia 98 huku ukitarajiwa kufunguliwa Rasmi Septemba 30 mwaka huu.
Mradi huo utakuwa na uwezo wa kusambaza umeme ndani ya Nchi pamoja na Nchi jirani.
Katika Mkoa wa Dodoma mahitaji ya umeme yameongezeka kutoka Megawati 20 hadi megawati 48.
Taswira ya habari imezungumza na meneja mradi wa kituo cha kufua umeme Zuzu Newton Mashimbwa na ameelezea hatua ya mradi huo ilipofikia.
Kituo cha kufua na kupoza umeme Zuzu Jijini Dodoma kinagharamiwa na Serikali kwa dola za marekani milioni 50 ili kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 48 hadi megawati 624 na kinatarajiwa kuwa kitovu cha umeme hapa Nchini.