Jamii imetakiwa kuacha mtazamo hasi juu umuhimu wa lishe bora
24 August 2021, 1:09 pm
Na;Yussuph Hans.
Jamii imekuwa na dhana mbalimbali juu ya umuhimu wa lishe bora ambapo dhana hiyo imesababisha baadhi ya watu kupendelea aina fulani ya chakula ili kukwepa gharama za vyakula vingine.
Wakizungumza na taswira ya Habari Wakazi Mkoani Dodoma wamesema kuwa baadhi yao wanadhani ili kula chakula chenye virutubisho lukuki lazima utumie gharama kubwa.
Aidha wameongeza kuwa kutokana na Elimu Duni kuhusu kula Chakula Bora imepelekea baadhi yao kutozingatia suala hilo ambapo ni hatari kiafya.
Kwa upande wake Afisa Lishe Jijini Dodoma Bi Semieva Juma amesema kuwa lishe bora ni muhimu sana katika kipindi hiki ili kuboresha kinga za mwili.
Kwa ajili ya afya bora ya mwanadamu, kuna umuhimu wa kula vyakula mbali mbali ambavyo huweza kuuweka mwili katika afya njema. Ukilinganisha na zamani, katika zama hizi watu wengi hukumbwa na matatizo mbali mbali ya kiafya ambapo vyakula tunavyokula huchangia kwa kiasi kikubwa.