Immelezwa kuwa wanawake wengi nchini hawazingatii unyonyeshaji wa watoto ipasavyo
17 August 2021, 12:29 pm
Na;Mindi Joseph .
Imeelezwa kuwa ni asilimia 58% ya wamama nchini ndio wananyonyesha watoto wao kikamilifu huku Watoto wengi wakikosa maziwa ya mama ipasavyo.
Akizungumza na Taswira ya habari Ruth Mkopi Afisa tafiti mwandamizi Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania amesema bado kuna changamoto kubwa ya wamama kunyonyesha watoto wao kwani hawazingatii unyonyeshaji.
Ameongeza kuwa kunauwezekano wa kupunguza vifo vya watoto laki nane na ishirinini ikiwa ni asilimia 12 endapo mama atazingatia kumnyonyesha kikamilifu mtoto wake katika miezi sita ya mwanzo.
Aidha Ameongeza kuwa watoto wanne tu kati ya 10 wananyonyeshwa maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo ya maisha yao sawa na asilimia 41 ya watoto wote kwa mujibu wa UNICEF mwaka 2018.
Katika maeneo ya vijijini inaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha kunyonyeshwa kuliko mijini.