Uongozi wa Chamwino watarajia kufanya maboresho ya miundombinu ya maji kijijini Msamalo
17 August 2021, 10:51 am
Na; Selemani Kodima.
Uongozi wa kata ya Msamalo wilayani Chamwino umesema unatambua uwepo wa changamoto ya maji katika kijiji cha Mgunga hivyo wanampango wa kufanya maboresho katika mtandao wa bomba za maji ili kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo
Akizungumza na Taswira ya Habari Diwani wa Kata ya Msamalo Bw Elias Kawea amesema kijiji cha mgunga kina Vyanzo vya Maji lakini hali ya miundombinu bado ni changamoto kutokana na uharibifu katika mitandao ya bomba za maji.
Aidha amesema vipo Vitongoji vingine ambavyo vimepitiwa na Mradi wa mwendokasi ambavyo hali ya upatikanaji wa maji ni changamoto na wanategemea kuwasiliana na mbunge wa jimbo la chamwino ili kuona uwezekano wa kuwachimbia Visima wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza Mpango wa kata ya Msamalo kuhakikisha wananchi wa maeneo mengine wanapata huduma ya maji amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni uchimbaji wa Visima vya maji katika baadhi ya Vijiji kutokana bajeti za Vijiji Husika.
Pamoja na hayo amesema Ushiriki wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni moja ya mbinu inayosaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili kutokana na msukumo wa Vikao na Usomaji wa mapato na matumizi.