Mashamba ya zabibu kuto guswa katika zoezi la upimaji ardhi Dodoma
26 July 2021, 10:59 am
Na;Mindi Joseph.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe.Jabir Shekimweri amesema Mkoa hautagusa mashamba ya kilimo cha zabibu wakati zoezi la upimaji wa viwanja likiwa linaendelea jijini Dodoma.
Akizungumza na Taswira ya habari Mh Jabir amesema Mkoa wa Dodoma wote unastahili kulimwa zabibu hivyo watahakikisha wanabakikisha mashamba ya zamani ya zabibu na wanatarajia kuongeza mashamba mapya ili kuendelea kuongeza zaidi uzalishaji wa zao hilo.
Ameongeza kuwa zabibu ni miongoni mwa mazao ya kimkakati na katika kuunga mkono agenda ya viwanda na uchumi watahakikisha zao hili linapewa kipaumbele zaidi.
Mh Jabir amesema hii ni fursa pekee kwa wananchi wa Dodoma kwani wakitilia mkazo zao la zabibu litawasaidia zaidi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kuombaomba.
Kilimo cha Zabibu Mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya usaidizi wa bihawana misheni, serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine.