Wakazi wa Chamwino walalamikia ukosefu wa huduma bora za Afya kwa watu wa makundi maalum
26 July 2021, 10:13 am
Na; Shani Nicolous.
Wakazi wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma wamelalamikia ukosefu wa huduma bora za afya kwa watu wa makundi maalumu kama wazee, watoto ,akina mama wajawazito na walemavu.
Wakizungumza na Dodoma Fm kupitia kipindi cha Dodoma live wamesema kuwa kumekuwa na changamoto ya huduma bora kwa kundi hili hali inayosababisha watu hawa wanakosa haki zao za msingi.
Wamesema kuwa wanaiomba serikali kuunda kamati mbalimbali za ufuatiriaji katika maeneo haya ili kusaidia upatikanaji wa huduma bure kwa watu wenye mahitaji maalumu hii itasaidia kubaini vitendo mbali mbali vya kukosa huduma bora kwa watu hawa.
Dodoma FM imezungumza na Mkuu wa Wilaya Chamwino Mh. Gifty Msuya amesema kuwa inawezekana kuna baadhi ya sehemu ukikwaji huo unatendeka hivyo kama Mkuu wa Wilaya anendelea kufanya ziara na kubaini baadhi ya changamoto katika Wilaya yake
Amewataka viongozi mbalimbali na wauguzi katika wilaya hiyo kuzingatia maelekezo ya serikali kwa kila jambo ambalo serikali inaelekeza vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Amewasihi wananchi wa wilaya hiyo kuripoti vitendo vya ukiukwaji wa haki kwenye vyombo vyake vikiwemo vya kisheria unaotendeka dhidi ya watu wa makundi maalumu na ikitokea kukosa ushirikiano kwa viongozi wa ngazi ya chini basi wapige simu kwenda namba 0757572767
Watu wa makundi maalumu wamekuwa wakilalamikia kukosa haki zao za msingi hususani katika huduma za afya na hii si kwa Chamwino peke yake bali hata kwa baadhi ya ameneo ambayo wananchi wamethibitisha kwa kupiga simu kupitia kipindi cha Dodoma live.