Wakazi wa Mlanje walalamikia uhaba wa walimu na na uchache wa vyumba vya madarasa
22 July 2021, 9:09 am
Na; Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Mlanje Kata ya Matongoro Wilaya ya kongwa wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya walimu wa shule ya msingi pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa uchache wa madarasa na upungufu wa walimu pamoja na nyumba za walimu imekuwa changamoto katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Elisha Mpanda amesema kuwa kupitia nguvu za wananchi wamejitahidi kujenga vyumba vya madarasa lakini walimu bado imekuwa tatizo kutokana na idadi ya wanafunzi kuwa kubwa ukilinganisha na walimu waliopo
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Jeremiah Makanda amekili kwa kutumia fedha za wananchi wamejitahidi kujenga maboma ya vyumba vya madrasa ila bado changaomoto kwa Serikali kwenda kuyamalizia.
Makanda ameongeza kuwa kutokana na umbali wa shule mama waliamua kujenga vyumba vya madarasa katika kijiji cha wenzamtima licha ya kukosa mwalimu hivyo kwasasa wameamua wanafunzi kukaa kambi kukabiliana na adha ya umbali.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi nchini ambalo linaendana na uchache wa walimu hali inayopelekea baadhi ya wazazi kuchangia kuwalipa walimu wa kujitolea