Wajasiriamali wanufaika na udhamini wa taasisi ya Pass Trust
22 July 2021, 6:25 am
Na;Mindi Joseph .
Takribani Wajasiriamali milioni 1.7 wamenufaika na udhamini wa taasisi ya Pass Trust ambayo imelenga kupunguza umasikini nchini kwa kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa wakulima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Kaimu Mkurungezi wa Pass Trust Annah Shanalingigwa amesema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo na serikali ya Tanzania na Denmark miaka 20 iliyopita ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha pass imeweza kudhamini miradi 46,300 yenye thamani ya shilingii trillion moja.
Ameongeza kuwa wanufaika wa udhamini huo asilimia 45 ni wanawake na wamefanikiwa kutengeneza fursa za ajira Takribani milioni mbili na nusu ambazo zimeboresha maisha ya watazania.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Jabir Shekimweri ameipongeza taasisi hiyo na kuwahakikishia ushirikiano na usalama wa uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.
Katika hatua nyingine Taasisi ya Pass Trust kwa kushirikiana na halimashauri ya jiji la Dodoma imeandaa mikutano ya wadau wa kilimo pamoja na uzinduzi wa kampuni ambayo itafanyika kuanzia katika viwanja vya mwalim nyerere kuanzia leo julai 22.