Wakazi wa Dodoma wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko 19
13 July 2021, 12:35 pm
Na; Shani Nicolous.
Wakazi jijini Dodoma wamehimizwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya uviko kwani ugonjwa huo ni hatari ulimwenguni kote.
Akizungumza na Dodoma fm Dr. Nassoro Ally Matuzya na maratibu wa elimu ya afya kwa umma mkoa wa Dodoma amesema kuwa Watanzania watambue uwepo wa gonjwa wa covid 19 na nivema wakazingatia hatua zote za kujikinga kutokana na maagizo ya mamlaka za afya na serikali.
Amesema kuwa wengi wao wanaacha kutumia barakoa kwa maana ya kutofahamu namna sahihi ya uvaaji na hivyo kama wataalamu wa afya hawana budi kutoa elimu sahihi juu ya uvaaji barakoa
Ikumbukwe kuwa moja kati ya njia ya kujikinga na ugonjwa huo ni pamoja na kuepuka misongamano pamoja njia nyingine ambazo zinaweza kuwa msaada kwa Watanzania kuepuka gonjwa hilo Mkuu wa Mkoa Dodoma Mh. Antony Mtaka ametoa maagizo namna ya kujikinga hususani katika vyombo vya usafiri Dodoma.
Ugonjwa wa corona ni hatari hivyo ni vyema jamii ikatambua umuhimu wakujikinga kwani endapo mtu akipata tunapoteza nguvu ya taifa kwa kupoteza watu kwa vifo , hivyo ni wajibu wakila mmoja kuzingatia kujikinga na ugonjwa huo kwa kuzingatia namna bora elekezi kutoka kwa wataalamu wa afya .