Dodoma FM

Wanafunzi wa vyuo watakiwa kujiandaa kisaikolojia kukabilia na changamoto ya ajira wanapo hitimu

5 July 2021, 10:54 am

Na;Yussuph Hans.

Mjadala kuhusu tatizo la ajira Nchini limekuwa likichukua sura mpya na hii ni kutokana na ukubwa wa tatizo hilo ambalo linaendelea kuumiza vichwa vya watungaji wa sera na wadau wengine.

Hali hii imepelekea baadhi ya wasomi na wachambuzi kuzilaumu taasisi za elimu kwa kudai kuwa zimeshindwa kuandaa wahitimu wao vizuri kulingana na matakwa ya soko la ajira.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali Jijini Dodoma, wamesema kuwa endapo Serikali itafanya maboresho ya mfumo wa elimu Nchini itasaidia kwa kiasi kikubwa wahitimu kukabiliana vyema na soko la ajira.

Kwa upande wake Dr. Aneth Komba pamoja na Godson Lema Wataalamu kutoka Wizara ya Elimu Taasisi ya Elimu Tanzania wamesema kuwa kumekuwa na utaratibu wa kubadilisha mitaala kila baada ya miaka kadhaa kulingana matakwa ya soko la ajira na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Hata hivyo baadhi ya walimu kutoka chuo cha uadishi wa habari na utangazaji Dodoma (DOMECO) wamesema ni vyema wanafunzi tangu awali wakajiandaa kisaikolojia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira na kutumia taaluma zao kwa kujiajiri.

Tatizo la upungufu wa ajira linatajwa kukithiri zaidi katika Nchi maskini ikilinganishwa na nchi tajiri, ingawa Nchi hizo pia zimekumbwa na tatizo hilo lakini Nchi tajiri pia zinatajwa kunufaika na mfumo wa uchumi wa ulimwengu.