Mkutano wa wadau kuchangia maoni uboreshaji wa mitaala ya elimu Nchini wafanyika Dodoma
26 June 2021, 3:07 pm
Na,Mindi Joseph .
Serikali imesmea ni vyema kusitisha mabadiliko yoyote kwenye mitaala ya Ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari iliyopo sasa Nchini mpaka mchakato wa wadau kuchangia maoni ili kuwa na Mtaala ambao ni shirikishi na jumuishi utakapokamilika.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa wadau wa elimu wa kukusanya maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala ya elimu Msingi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga, amesema kuwa pamoja na mitaala inayotumika kwa sasa nchini kuendelea kufanya vizuri bado kuna Haja ya kuboresha mitaala inayotumika shuleni ili ielekezwe kwenye kutoa elimu ya ujuzi zaidi itakayowezesha wahitimu kujitegema na kutumia fursa zilizopo nchini.
Mh Kipanga ameongeza kuwa Lengo la maabadaliko ya mitaala ni kuendena na hali halisi na mpaka sasa mabadiliko makubwa ya mitaala ya elimu msingi yamefanyika mara tano tangu Tanzania kupata uhuru mwaka 1961.
Aidha Mh kipanga ameipongeza Taasisi ya elimu tanzania TET kwa kuwakutanisha wadau wa elimu katika Mkutano muhimu wa kutoa maoni ya uboreshaji wa mitaala ya elimu ya awali,msingi na sekondari .
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amesema Wizara itahakikisha inasimamia mchakato wa uboreshaji wa mitaala ya Elimu ya awali msingi na sekondari kwani ni Muhimu katika kusaidia kukidhi mahitaji ya tanzania ya uchumi wa kati na ujenzi wa viwanda.
Mkutano wa kupoke maoni ya wadau kuhusu uboreshaji wa elimu ya awali msingi na sekondari umefanyika leo jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano ya jakaya kikwete convetional center na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu nchini.