Wananchi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufuatilia elimu ya katiba
3 June 2021, 11:44 am
Na; Shani Nicolous.
Wito umetolewa kwa wananchi nchini kufuatilia elimu zinazotolewa juu ya katiba ya nchi ili kuwawezesha kutambua haki na sheria mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Bw. William Mtwazi kutoka katika kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wakati akizungumza na Dodoma fm amesema kuwa elimu hiyo itawasaidia kufahamu haki zao za msingi pamoja na kushiriki katika maamuzi mkubwa ya kitaifa.
Aidha amesema kuwa kituo hicho kimejiandaa vema kutoa elimu kwa wananchi kuhusu katiba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kutumia fursa hii ili kutengeneza uelewa utakao muwezesha kuchangia maamzi mbalimbali juu ya katiba nchini.
Dodoma fm amezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dodoma ambao wamesema kuwa ni vyema elimu hii itolewe kwa wingi vijijini kwani watu wengi hawana uelewa juu ya katiba.
Ili kutengeneza nchi yenye miongozo bora amani na mshikamano wananchi wametakiwa kuwa na kiu ya kufahamu mambo mengi hasa yahusuyo miongozo mbalimbali inayoweza kuwatengenezea maisha mazuri na kufurahia utawala bora katika nchi husika.