Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanatimiza malengo
1 June 2021, 1:46 pm
Na; Shani Nicolous.
Kuelekea siku ya mtoto wa Afrika juni 16 shirika la Mercy Empowerment Foundation limeandaa kambi ya watoto ya siku tatu kwaajili ya kuwafundisha stadi za kazi.
Mercy Empowerment Foundation ni shirika linalojihusisha na masuala ya watoto, Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu
Akizungumza na Dodoma fm mkurugenzi wa shirika hilo Mchungaji Mercy Ghadwe amesema kuwa kambi hiyo itajumuisha watoto wenye umri tofauti ili kuwajengea misingi mbalimbali ya kimaisha.
Kiongozi huyo amesema makundi ni kati ya suala linaloweza kumbadilisha mtoto na hata kupoteza malengo kwa kutofanya chaguo sahihi hivyo kama wazazi na walezi ni jukumu lao kuhakikisha mtoto anafikia malengo yake.
Aidha ameongeza kuwa miongoni mwa mambo watakayofundisha ni pamoja na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka kuitumia vibaya kama zilivyo jamii nyingi kwa sasa.
Msingi bora wa tabia ya mtoto hujengwa na mzazi hivyo ni vema wazazi wakawa karibu na watoto wao ili kumtengeneza tangu akiwa mdogo.