Wananchi wametakiwa kufichua mambo yanayo kiuka haki za binadamu
20 May 2021, 1:27 pm
NA ;SHANI NICOLOUS.
Wananchi wametakiwa kufichua mambo ambayo ni uvunjivu wa sheria inayokiuka haki za binadamu na utawala bora .
Wito huo umetolewa na Mohamed Hamis ambaye ni makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora wakati akizungumza na Taswira ya habari ambapo amesema wananchi wanao wajibu wa kukuza nakuendeleza haki za binadamu kwa kutii sheria za nchi nakushirikiana na mashirika mbalimbali ili kujenga jamii inayo zingatia haki za binadamu.
Amesema wananchi ndio wenye nguvu za kutoa ushirikiano na tume hiyo kwa kutoa taarifa zitakazosaidia uchunguzi wa masuala mbalimbali yatakayo ondoa na kukukomsha masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ameongeza kuwa wanatambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali zainazohusiana na haki za binadamu ambazo hushirikiana nazo na tayari mikataba mbalimbali imefanyika huku wakifanya mikutano na kutambua mafanikio ya ushirikiano huo ambapo mafanikio mengi yanaonekana kwa kufanya kazi kwa pmoja.
Dodoma fm imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dodoma ambapo wamesema kuwa tume ya haki za binadamu na utawala bora inapaswa kutembelea maeneo mbalimbali hususani vijijini ili kutoa elimu kwa wananchi husika juu ya haki za binadamu.
Kila binadamu ana haki zake hivyo ni vema kufuata sheria za mahali husika pamoja na kuzitumia kwa nidhamu kwa kufuata taratibu na sheria za mahali husika.