Wafugaji watakiwa kutumia njia bora za ulishaji wa mifugo
10 May 2021, 11:24 am
Na; Thadei Tesha.
Wafugaji nchini wameshauriwa kutumia njia bora za kisasa na kiteknolojia za kulisha mifugo ili kuleta tija katika soko la mifugo nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum na kipindi cha taswira ya habari mtaalamu na mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa mifugo nchini TALIRI Bw.Alfredy Ossena amesema wakulima wengi wanapaswa kutumia njia bora na za kisasa katika kulisha mifugo yao ili iweze kuleta tija kibiashara.
Aidha Bw.Ossena ametoa wito kwa wafugaji kuendelea kujifunza masuala mbalimbali ya utafiti wa mifugo ambapo wamesema TALIRI itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala hilo.
Kwa upande wao baadhi ya wafugaji jijini hapa wamesema elimu inayotolewa na taasisi mbalimbali za utafiti imekuwa ikiwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata mazao ya kutosha yanayotokana na mifugo.
Ufugaji ni miongoni mwa sekta ambazo zimewasaidia wananchi wengi kujikwamua kiuchumi kutokana na kuajiri watu wengi nchini.