WWF yaishukuru Serikali kwa kushiriki juhudi utanzaji wa Mazingira
30 April 2021, 9:36 am
Na; Benard Filbert.
Shirika la uhifadhi wa mazingira Duniani (WWF) limeishukuru serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya utunzaji wa mazingira nchini hali ambayo imesaidia kuboresha mazingira kwa kiasi kikubwa.
Hayo yamesemwa na Afisa mawasiliano kutoka shirika hilo Bi Joan Itanisa wakati akizungumza na taswira ya habari kufuatia shirika hilo kutimiza miaka 60 katika kuhudumia jamii katika suala la uboreshaji wa mazingira.
Amesema serikali imekuwa ikiunga mkono juhudi za shirika hilo kutokana na mlengo wake wa kuboresha mazingira toka shirika hilo lilipoanzishwa hadi hivi sasa.
Akizungumzia mafanikio ya Shirika hilo Bi. Joan amesema shirika hilo linatimiza miaka 60 likiwa limefanikiwa kushirikiana na taasisi mbalimbali hapa nchini katika kuhifadhi mazingira.
Shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira ulimwenguni (WWF)limetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake huku likiwa limefanikiwa kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi mbalimbali.