Wazazi waiomba Serikali na Taasisi za Elimu kutilia mkazo somo la stadi za kazi na maisha kwa wanafunzi
22 April 2021, 12:19 pm
Na ; Mariam Kasawa
Wazazi jijini Dodoma wametoa wito kwa Serikali na taasisi za elimu nchini kutilia mkazo ufundishwaji wa masomo ya stadi za kazi na maisha ili kuwafanya wanafunzi kuwa na haiba nzuri pamoja uwezo wa kufanya kazi pindi watakapohitimu.
Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wazazi hao wamesema somo la stadi za kazi linapaswa kutiliwa mkazo shuleni ili kuwaandaa wanafunzi na kuwafanya wachapakazi pindi watakapohitimu masomo yao.
Kwa upande wao baadhi ya walimu katika shule mbalimbali jijini hapa wamesema wamekuwa wakitumia mbinu rafiki ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu na maarifa.
Somo la stadi za kazi na maisha limekuwa likifundishwa katika shule mbalimbali ambapo serikali imetakiwa kutilia mkazo ili kujenga Taifa la watu wanaojituma katika kazi.