Mlowa Bwawani kufikisha huduma ya maji katika maeneo yake ambayo hayajafikiwa
22 April 2021, 11:25 am
Na; Benard Filbert
Kufuatia kukamilika kwa marekebisho ya mradi wa maji katika Kata ya Mlowa Bwawani Wilayani Chamwino, uongozi wa Kata umejipanga kufikisha huduma hiyo kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa.
Hayo yanajiri kufuati miezi kadhaa iliyopita mradi huo kushindwa kufanya kazi vizuri kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa nishati ya kuvuta maji kwenye kisima.
Akizungumza na Dodoma fm Diwani wa Kata ya Mlowa Bwawani Bw.Andrew Richard amesema kilichosababisha mradi huo kutofanya kazi hapo awali ni ukosefu wa nishati ya umeme wa jua baada ya kutokea kwa shoti.
Bw.Andrew amesema mkakati uliopo kwa sasa ni kuhakikisha wanafikisha huduma ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na tayari wadau wamepatikana kwa ajili ya kazi hiyo.
Huduma ya maji katika katika Kata ya Mlowa Bwawani ilikuwa ikisuasua kutokana na kuharibika kwa mfumo wa nishati ya umeme wa jua lakini kwa sasa wameunganishiwa umeme wa TANESCO.