DUWASA kukabiliana na wezi wa maji Dodoma
13 April 2021, 1:16 pm
Na; Mindi Joseph
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira( Duwasa) kukabiliana na wezi wa maji na uvujifu wa maji pamoja na kuwachukulia hatua watumishi wa Duwasa wasio waminifu wanaochangia hasara katika Mamlaka hiyo.
Akizungumza mapema leo hii katika semina ya wenyeviti na Watendaji wa Mitaa Jijini Dodoma amesama kuwa baadhi ya watumishi katika mamlaka hiyo sio waaminifu wanaingiza hasara ya mapato kwa kushirikiana na wananchi hivyo ni vema wakawachukulia hatua pamoja na kudhibiti wezi wa maji.
Aidha Dkt. Mahenge ameipongeza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Duwasa) kwa jitihada kubwa inayofanya kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya maji kwani hadi sasa jiji la Dodoma lina upugufu wa maji Zaidi ya lita million 37 kufuatia uzalishajii wa maji wa lita Milion 103.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Duwasa) Profesa Faustine Bee Mwenyekiti UWT Mkoa wa Dodoma Bi.Neema Majule amesema maji ni kapaumbele na Duwasa imefanya kazi kubwa kukidhi mahitaji ya maji kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dodoma.
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Antony Mavunde amebainisha kuwa Kuanzia mwezi wa 11 hadi sasa visima 10 vya maji vimechimbwa kati ya visima 20.
Kukamilika kwa miradi miwili ya maji jijini Dodoma Mradi wa Farkwa na ziwa victoria itasaidia kuondoa adha ya maji kwa wananchi Dodoma.