Marufuku ya vifungashio kufika tamati Kesho Aprili 9
8 April 2021, 9:28 am
Na; Mariam Matundu
Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya kuwepo kwa vifungashio visivyokidhi viwango vya ubora sokoni ,vifungashio vipya vinavyokidhi viwango vya ubora tayari vimeanza kupatikana sokoni.
Hayo yamezungumzwa na Afisa mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Anamaria Gerome ambapo amesema wamefanya ziara katika baadhi ya masoko makubwa hapa Dodoma na kuvikuta vifungashia hivyo vyenye ubora vikiwa vimeanza kutumika.
Amesema kuanzia kesho hawatarajii kuona vifungashio visivyokidhi wiwango vya ubora sokoni na kwamba operation maalumu itafanyika kuanzia kesho Nchi nzima kukagua iwapo bado kuna wafanyabishara wanatumia vifungashio hivyo.
Baadhi ya wananchi bado wana wasiwasi iwapo vifungashio vipya vitakuwa na bei rafiki kwa wafanyabiashara na kuomba suala hilo liangaliwe vizuri.
Hayo yamefuatia muda wa siku tisini ulitolewa na aliyekuwa waziri ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira Mh. Ummy Mwalimu ambapo alitoa marufuku ya utengenezaji na usambazaji pamoja na matumizi ya vifungashio vya plastic sokoni agizo hilo lilitolewa januari 8 na mwisho wake ni hapo kesho Aprl 9