Wananchi waaswa kuto tumia shughuli za kibinadamu kuharibu barabara.
6 April 2021, 12:52 pm
Na; Mariam Matundu.
Barabara ya Makanda Kintinku iliyokuwa imepoteza mawasiliano tangu mwezi decemba mwaka jana imeanza kufanyiwa ukarabati ambapo hatua mbalimbali za awali zinaendelea.
Akizungumza na tawsira ya habari manager wa Tarura wilaya ya Manyoni bw. Yose Mushi amesema zoezi la kuinua tuta lenye urefu wa kilometa moja linaendelea na baadae ujenzi wa madaraja mengine ambapo wanatarajia hadi mwezi mei kukamilisha ukarabati wote.
Bwana Mushi amewasisitiza wananchi hasa wakulima na wafugaji kutokutumia shuguli zao za kilimo na ufugaji kuharibu miundombinu kwakuwa uharibifu wa barabara hiyo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu.
Nae diwanai wa kata ya Makanda bw. Jumanne Mlagaza amewaomba Tarura kuharakisha ukarabati wa barabara hiyo ambapo amesema barabara hiyo inatakiwa kupata suluhisho la kudumu kwani imekuwa ikisababisha adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo wakati wa kipindi cha mvua .
Mwezi wa pili mwaka huu taswira ya habari iliripoti changamoto ya Barabara ya makanda –kintiku yenye urefu wa takribani kilometa 31 ambayo imekuwa ikileta changamoto kila wakati wa masika na kusababisha adha kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo hivi sasa hatua zimeanza kuchukuliwa.