Dodoma FM

Wasiolipa ada ya usafi jijini Dodoma kukiona

11 February 2021, 2:00 pm

Na,Yusuph Hans,

Dodoma.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imeelezea baadhi ya adabu anazoweza kupewa mwananchi au kaya ambayo haitaki kulipa ada ya uzoaji taka, inayokusanywa kutokana na huduma hiyo kutolewa kila wiki.

Akizungumza na Taswira ya Habari afisa afya wa Jiji la Dodoma Abdallah Mahia amesema kumekuwepo na kesi nyingi za baadhi ya wananchi kutokulipa ada za ukusanyaji wa taka, hali inayorudisha nyuma utendaji kazi wa Kampuni ya usafi ya Green Waste inayotoa huduma hiyo.

Aidha Bwana Mahia amesema kuwa kulipa Ada ya ukusanyaji Taka kila mwezi ni Haki ya kila Mwananchi na kusisitiza kuwa suala la usafi kwa kila siku za Jumamosi ni muhimu katika kuweka jiji Safi.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste yenye zabuni ya uzoaji taka jijini Dodoma wakiendelea na kazi yao

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa kuhusiana na Changamoto zinazojitokeza wakati wa ukusanyaji taka ambapo wasema kuwa wakati mwingine taka hukaa muda mrefu bila kuchukuliwa, hali inayosababisha kusambaa hovyo.