Dodoma FM

Ushirikiano mdogo wachochea vitendo vya ukatili

4 February 2021, 1:51 pm

Na,Alfred Bulaya,

Dodoma.

Imeelezwa kuwa ushirikiano mdogo baina ya mamlaka zinazoshughulikia masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto, ni moja ya chanzo cha kuongezeka matukio hayo hali inayodhohofisha jitihada za kukomesha vitendo hivyo.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto ngazi ya Taifa MTAKUWWA Bw.Joel Mangi wakati akizungumza na Taswira ya habari baada ya kikao na wajumbe wa kamati hiyo ngazi ya halmashauri, kilichoandaliwa na shirika la WOWAP Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Mratibu wa dawati la maendeleo ya mtoto Wilayani humo Bi.Sophia Swai amesema wilaya ya Chamwino imekuwa moja ya maeneo yaliyo na matukio mengi ya ukatili kwa watoto huku kesi nyingi zikitatuliwa kifamilia hali inayochangia vitendo hivyo kuendelea.

Kwa upande wake mratibu wa miradi kutoka shirika la WOWAP Nasra Suleiman ametoa wito kwa wanakamati walioshiriki kikao hicho kuhakikisha wanafanyia kazi mikakati na maazimio yaliyofikiwa na MTAKUWWA kwa ngazi ya halamshauri, Kata na Vijiji.