Dodoma FM

PROF.Nchembe:Idadi ya vyoo bora nchini yaongezeka 2020

16 December 2020, 3:06 pm

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe akifungua Mkutano wa Maafisa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.

Na,Mindi Joseph,

Dodoma.

Idadi ya vyoo bora nchini imeongezeka kutoka asilimia 62.4 kwa mwaka 2019 hadi asilimia 64 kwa mwaka 2020.

Hali hii imechangiwa na usimamizi bora uliofanyika kupitia kampeni ya nyumba ni Choo ambayo inafanyika nchi Nzima kwa lengo la kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora kwa wananchi kwa kipindi cha miaka 3.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa afya Tanzania bara Katibu Mkuu Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dk Mabula Mchembe amesema licha ya mafanikio hayo amewataka Maafisa afya kufanya kazi kwa kusimamia maadili ili kutatua baadhi ya

Maafisa Afya kutoka maeneo ya mipaka wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tathmini wa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Balozi wa kapeni ya nyumba ni choo Mrisho mpoto Mapema leo akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kinachorushwa hapa Dodoma Fm amebainisha kuwa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo imepiga hatua katika ujenzi wa vyoo kupitia kampeni ya nyumba ni choo.

Balozi wa kampeni ya nyumba ni choo “usichukulie poa” Mrisho Mpoto “Mjomba” akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya Studio za Dodoma Fm Radio hii leo

Ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa afya Tanzania bara 2020 umefanyika hapo jana na kilele chake kitakuwa siku ya ijumaa ya Decemba 18 huku ukibebwa na kauli mbiu isemayo “Zinagatia mahitaji ya jinsia kwa usafi wa mazingira Endelevu”.