Bozizé akosa sifa ya kuwania Urais C.A.R
4 December 2020, 10:33 am
Bangui,
C.A.R.
Mahakama ya Katiba imethibitisha uamuzi wa Tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé , hana nafasi ya kuwania urais katika uchaguzi wa Desemba 27 nchini humo.
François Bozizé anashtumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na mateso bila kusahau vikwazo alivyowekewa na Umoja wa Mataifa.
François Bozizé, aliye kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2003 hadi 2013, alitangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi ujao dhidi ya rais anayemaliza muda wake, Faustin-Archange Touadéra.
Waranti wa kimataifa wa kukamatwa ulitolewa dhidi yake na mahakama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini amekuwa hana wasiwasi tangu kurudi kwake kutoka uhamishoni.