Gwiji wa Manchester United Gary Neville ailaumu FA
4 December 2020, 9:43 am
Manchester,
England.
Gwiji wa Manchester United Gary Neville ametoa wito kwa chama cha soka England FA kutoa mafunzo maalum kwa wachezaji wanaohamia kucheza katika klabu mbalimbali za ligi kuu ya primia huku akilaumu chama hicho kwa kutofanya hivyo.
Kauli ya Neville inakuja siku chache baada ya mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavani kuchapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram ukitafsiriwa kuwa ni wa kibaguzi na baada ya muda mfupi kuufuta.
Baada ya kufunga mabao mawili katika mechi ya ligi dhidi ya Southampton wakitoka nyuma 2-0 na kushinda 2-3,Cavani alichapisha ujumbe wa kupongeza ukisomeka Gracias Negro”Ahsante/hongera mtu mweusi”.
“Walakini wachezaji wanapaswa kupitia mafunzo ya ujumuishaji ili kuwaelimisha juu ya utofauti na ubaguzi” amesema Neville na kuongeza
“Tunasikia neno elimu na mafunzo na bado mpira hauwezi kuweka mtaala mahali kwa wachezaji wake, kwa wanachama wake, kwa mashabiki wake ambayo ni lazima,”
Chama cha soka England FA kimetangaza kufanya uchunguzi juu ya ujumbe huo wa Cavani.