Dodoma FM
Dodoma FM
23 February 2026, 5:37 pm

Hata hivyo tayari wamekwisha peleka ombi Halmashauri Ili waweze Kufanya zoezi la utambuzi kabla ya kulipima upya eneo hilo na kulikabidhi kwa kijiji.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Mapinduzi Akata ya Ngh’ongh’ona wameiomba serikali kuingilia kati watu walio vamia eneo lao la kimila .
Wameeleza kuwa ni takribani miaka hamsini eneo hilo limekuwa mali ya jamii nzima na sio mtu mmoja lakini kwasasa wanashangaa kuona eneo hilo linagawanywa vipande vipande na kupewa watu.
Wananchi hao wameongeza kuwa ni vyema eneo hili kuchukuliwa mikononi mwa walio livamia Ili kuwa fiadi ya jamii yote Kwa ujenzi wa vyanzo mbalimbali vya huduma za kijamii.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi A Bw.Golden Mathayo amesema kuwa ni kweli kumekuwa na changamoto ya uvamizi wa eneo la kimila katika mtaa huo.
Ameongeza kuwa hata hivyo tayari wamekwisha peleka ombi Halmashauri Ili waweze Kufanya zoezi la utambuzi kabla ya kulipima upya na kulikabidhi mikono ya Serikali ya kijiji.