Dodoma FM
Dodoma FM
26 January 2026, 5:26 pm

Awamu ya mwisho ya mradi huo ilitamatika tangu mwezi Septemba mwaka jana hivyo wanasubiri awamu nyingine kama watapata fursa ya kusajili kundi lingine la wazee wasiojiweza.
Na Victor Chigwada.
Kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wazee wa kijiji cha Msanga, wilaya ya Chamwino jijini Dodoma wameiomba serikali kuwasaidia kupata msaada kupitia mfuko wa kusaidia kaya masikini TASAF.
Baadhi ya wazee hao wamesema mfuko huo ulipokuja kwa awamu ya mwisho, baadhi yao hawakusajiliwa kutokana na madai ya kukosa sifa, hivyo wamekuwa wakipitia maisha magumu hasa pindi wanapohitaji huduma za afya.
Shirika la HelpAge Tanzania (shirika la kiraia lenye utafiti wa masuala ya wazee) linaonyesha kwamba kupitia juhudi za ulinzi wa kijamii, TASAF limewezesha kujiunga kwa wazee 574,608, ambapo kati yaowazee 316,034 ni wanawake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha Msanga Hatibu Ally amesema uwepo wa mradi wa TASAF umewasaidia wazee wasiojiweza kuendesha maisha yao, ingawa mradi huu haukuweza kunufaisha kata za eneo zima hivyo baadhi ya wazee wakiachwa kwa kusubiri awamu nyingine