Dodoma FM

Wananchi Msanga walalamikia magari yanayobeba mchanga

21 January 2026, 2:59 pm

Picha ni gari limebeba mchanga. Picha na Blog.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa  mbali na mwendo mkali, magari hayo pia yamekuwa chanzo cha vumbi ambalo huathiri biashara za wananchi .

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Msanga wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamelalamikia magari yanayobeba mchanga kutembea kwa mwendo kasi, jambo ambalo linahatarisha usalama wa wananchi hususani watoto.

Akizungumza na taswira ya habari, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Msanga Ndg. Hatibu Ally amesema magari hayo mara kadhaa yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na madereva wa magari hayo kuendesha kwa mwendo mkali na kushindwa kuzingatia alama za barabarani

Sauti ya Hatibu Ally.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Msanga, wamesema kuwa uwepo wa vumbi umekuwa ukisababisha changamoto kwenye biashara zao na kuathiri afya zao.

Sauti za wananchi.